Featured Post

This city is known as Dar es salaam, a business center of Tanzania, Located in East Africa

This city is known as Dar es salaam       This city is known as Dar es salaam, the business city of Tanzania, Located in East Afri...

Saturday, August 17, 2013

MWAKYEMBE - "HIVI NDIVYO CCTV ZILIVYOWANASA AKINA MASOGANGE"

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana ameanika majina ya watu saba waliohusika kupitisha mabegi tisa yaliyokuwa na kilo 180 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh8 bilioni, Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwamo maofisa usalama wanne wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na polisi mmoja.
Alisema mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa kutumia mbwa wa Idara ya Usalama wa Taifa, lakini siku ya tukio hilo mbwa hao walichelewa na walitumika baada ya mizigo kuingizwa kwenye masanduku ya chuma.
“Kwa abiria watatu kuwa na mabegi makubwa tisa yanayofanana si kitu cha kawaida kukwepa jicho la maofisa wa ushuru wa forodha na vyombo vya usalama, sijui walikuwa wapi siku hiyo?” alihoji Dr. Mwakyembe.

Majuzi waziri huyo aliahidi kuyaweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini, na alitekeleza ahadi hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, kusema kuwa watu hao wamenaswa baada ya mfumo wa kamera (CCTV) za uwanja huo kudaka matukio kadhaa yaliyotokea siku ya tukio hilo, kuanzia saa 9:25 hadi saa 10:30 alfajiri.
Ameagiza wafanyakazi hao wanne pamoja na askari polisi mwenye cheo cha koplo, mbeba mizigo na mfanyabiashara aliyekuwa na wasichana wawili waliokamatwa Afrika Kusini, (ambao hatuwezi kuwataja kutokana na kushindwa kuwapata kujieleza) kuchukuliwa hatua za kinidhamu, kukamatwa na kuunganishwa na watuhumiwa waliokwenda na mzigo huo Afrika Kusini.
Mabegi hayo yaliyokuwa na dawa za kulevya aina ya ‘Crystal Methamphetamine’, yalipitishwa na wasichana wawili wasanii aliowataja kuwa ni Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa Edward ambao walidakwa siku hiyohiyo katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Afrika Kusini na tayari wameshafikishwa mahakamani.

Majuzi Dk Mwakyembe alifanya ziara JNIA kukagua utendaji kazi kwenye uwanja huo ikiwa ni siku tatu baada ya ahadi aliyotoa akiwa Mwanza kwamba katika kipindi cha wiki mbili, atahakikisha anawakamata vigogo wote walio katika mtandao wa usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vyote vya ndege nchini.
Saa nane baada ya ziara hiyo, Maofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wanadaiwa kumkamata Edwin Monyo akiwa na kete 86 za dawa aina ya heroini na misokoto 34 ya bangi aliyokuwa akiisafirisha kwenda Italia kupitia Zurich.

Mwakyembe asimulia jinsi vijana na MFANYABIASHARA huyo walivyonaswa na Camera za siri CCTV katika uwanja huo wa JNIA

Mwakyembe alisema kamera za CCTV, zilizowekwa uwanjani hapo
zinaonesha mchezo mzima ulivyokuwa.
Alisema majira ya saa 10:15 walionekana Agnes ‘Masogange’ Gerald
akiwa na mdogo wake Melisa Edward walionekana wakiwa na
mfanyabiashara mmoja katika eneo la kuingilia abiria huku wakiwa na
mizigo na mabegi tisa yaliyofanana.
Alisema kamera zilimwonyesha askari polisi akihangaika kuwasaidia abiria
mbalimbali kuweka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi, kazi
ambayo alieleza kuwa haikuwa yake.
“Mbeba mizigo anayetuhumiwa kuwa katika mtandao huo alionekana
akiwasaidia vijana hao watatu (Agnes, Melisa na mfanyabiashara)
kupeleka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi na baadaye
kuyazungushia mabegi hayo katarasi za nailoni na kuyafikisha kaunta ya
Shirika la Ndege la Afrika Kusini,” alisema.
Alisema kamera hizo zilimnasa ofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania, TAA akimwondoa katika kiti cha ukaguzi wa mizigo
mfanyakazi mwenzake, na kukaa yeye ikiwa ni dakika chache kabla ya
mabegi tisa ya vijana hao hayajaingia katika mashine ya ukaguzi.
“Kinyume na taratibu ofisa huyo hakujiandikisha kwenye kitabu cha
wakaguzi (Screener’s logbook), saa 10:16 akaanza kupitisha mabegi
hayo tisa mpaka saa 10:22. Alipomaliza kupitisha mizigo hiyo kwa
dakika sita akamwachia ofisa aliyekuwa katika eneo hilo na kuondoka.”
Dr Mwakyembe alidai ofisa huyo baada ya kuondoka katika kiti hicho
alizungumza kwa dakika kadhaa na askari polisi anayedaiwa kuwa katika
mtandao huo na kurejea tena sehemu aliyokaa ofisa mwenzake wa
TAA na kumnong’oneza jambo fulani.
“Baada ya hapo akaelekea ukumbi wa abiria huku akiongea na simu,
mambo hayo yote yalifanyika huku kiongozi wa sehemu ya ukaguzi
akiwa hapohapo bila kushtuka.”
Alisema baada ya mizigo hiyo kupita katika mashine ya ukaguzi (baggage
screening machine), vijana wale watatu wakahamia na mizigo yao
kwenye kaunta ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
“Mabegi matatu ya kilo 20 kila moja yalipitishwa yakabaki mabegi sita
ambayo yalitakiwa yalipiwe malipo ya uzito wa ziada. Kwa taratibu za
shirika hilo kila kilo moja inayoongezeka hulipiwa dola 5 (Sh8,000),
vijana wale walitakiwa kulipia dola 600, lakini walitozwa dola 94 tu
ambazo zinathibitishwa na risiti tuliyonayo,” alisema.
Alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye
hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo
hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia
gharama ya dola 60 (Sh96,000) ili kupata tiketi.
“Kutokana na hali hiyo mhakiki wa nyaraka za safari nje ya ukumbi wa
abiria siku hiyo, hakupaswa kumruhusu mfanyabiashara kuingia ndani ya
ukumbi bila tiketi ya siku hiyo,” alisema na kuongeza; “Kwa hali ya
kawaida mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa
kutumia mbwa, lakini siku hiyo mbwa walichelewa na walikuja kutumika
baadaye ikiwa ni baada ya mizigo kuingizwa kwenye masanduku ya
chuma.”
Alisema siku ya tukio saa 9:28 kamera hizo za usalama zilimwonyesha
mbeba mizigo wa uwanja huo akiwa anazungukazunguka eneo la
kuingilia abiria kama mtu ambaye ana ahadi na kukutana na mtu fulani.
“Kamera pia zilimnasa ofisa mwingine wa TAA kwa mara kadhaa
akitoka na kuingia ndani ya jengo la abiria huku akizungumza na simu,
kitendo ambacho hakiruhusiwi kabisa kwa wafanyakazi wa eneo la
ukaguzi wa abiria,” alisema na kuongeza;
“Wakati huohuo, kamera zilikuwa zinamwonyesha askari polisi
anayetuhumiwa kuhusika katika mpango huo akiwa anarandaranda eneo
la uhakiki wa hati za kusafiria kama vile anasubiri kitu fulani.”
Kutokana na hali hiyo, Dr. Mwakyembe ameliagiza Jeshi la Polisi
kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata
mfanyabiashara anayedaiwa kuwasaidia Masogange na mwenzake
kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya
dawa hizo huko Afrika Kusini, “Akamatwe na kuunganishwa na kesi
inayowakabili Watanzania hao wawili.”
Alisema TAA inatakiwa kuwafukuza kazi mara moja wafanyakazi
wake wanne waliohusika katika mpango huo, kuwakamata na
kuwaunganisha katika mashtaka yanayowakabili


“Serikali imeziagiza taasisi zote zilizopo chini ya JNIA kutekeleza majukumu ipasavyo na kwa mujibu wa sheria na taratibu ili kuhakikisha dawa za kulevya hazipiti kwenye kiwanja hicho kikuu cha ndege nchini,” alisisitiza.


No comments:

Post a Comment