Mshambuliaji anayetaka kuondoka Anfield LUIS SUAREZ amesema hana mpango wa kuomba msamaha kwa klabu yake ya Liverpool
Mchezaji huyo ambaye sasa ameamriwa kufanya mazoezi peke yake tangu alipokorofishana na uongozi wa timu yake kufuatia madai ya timu hiyo kumuahidi kuondoka iwapo watashindwa kupata nafasi ya LIGI YA MABINGWA ULAYA
Meneja wa Reds, Brendan Rodgers alikaririwa akisema mchezaji huyo anapaswa kuomba msamaha kwa kuidhalilisha klabu hiyo.....lakini SUAREZ amesema Haoni kibaya alichokifanya na Hana mpango wa kuomba msamaha kwa kuwa hakuna utovu wa nidhamu wowote alioufanya
No comments:
Post a Comment