Tarehe 20/08/2013
Release No. 137
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 20, 2013
Jumla
ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi
mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika
Oktoba mwaka huu.
Kwa upande wa TFF waliorejesha fomu kwa
upande wa urais ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari
Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura. Nafasi ya Makamu wa Rais
wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan na Walace Karia.
Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha
kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Odessa
Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Vedastus Kalwizira Lufano, Samwel
Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko, Stanslaus Haroon
Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii.
Ahmed Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi
Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja, Ayoub Shaib
Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud
Peter Mvela, John Mwachendang’ombe Kiteve, James Patrick Mhagama,
Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge.
Athuman Kambi, Francis Kumba Ndulane,
Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Ernest Masima,
Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange, Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki,
Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed.
Wengine ni Alex Chrispine Kamuzelya,
Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda
Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.
Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee.
Kwa upande wa TPL Board waliojitokeza
kuwania uongozi wa juu ni wawili tu; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na
Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).
Walioomba nafasi za ujumbe wa TPL Board
ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu
Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment